Alhamisi 17 Septemba 2026 - 00:30
Chuo Kikuu cha Marekani chawapiga marufuku wanafunzi wa Kiislamu kuswali

Hawza/ Chuo Kikuu cha Marekani cha New York, katika tawi lake la kampasi ya Lebanon, hivi karibuni kimewapiga marufuku wanafunzi wake wakiislamu kuswali.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma Shirika la Habari la Hawza, makao makuu ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Lebanon yaliyopo New York, wanafunzi wa kampasi ya mji wa Byblos wanasema kuwa wanazuiwa kuswali. Ukosefu wa nafasi ya kuswalia katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Lebanon mjini Byblos umeibua mjadala na utata nchini Lebanon, wanafunzi Waislamu wanakituhumu chuo hicho kwa kuwabagua.

Byblos, inayojulikana pia kwa jina la Jbeil, ni mji wenye wakazi wengi Wakristo ulioko kaskazini mwa Beirut, lakini mamia ya wanafunzi Waislamu wanasoma katika kampasi ya chuo hicho.

Wanafunzi wengi, wakiwemo hata wasio Waislamu, wamekituhumu chuo hicho kwa kuwazuia wanafunzi Waislamu kuswali katika maeneo ya chuo na kufunga maeneo yaliyokuwa yakitumika hapo awali kwa ajili ya kuswalia ndani ya chuo. Pia wameeleza kuwa hakuna msikiti ulio karibu na chuo ambao mtu anaweza kuufikia kwa kutembea, na kwamba kufika misikitini kunahitaji muda.

Baada ya kufungwa eneo la kuswalia, chuo pia kimechukua hatua dhidi ya wanafunzi wanaoswali katika sehemu nyingine yoyote, mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho, ambaye alitaja jina lake la kwanza pekee, Suleiman, aliliambia gazeti la New Arab: «Wanafunzi walikuwa wakiswali katika chumba cha kubadilishia nguo ambacho hakikuwa kikitumika, lakini chuo kilisema kuwa kinataka kukibadilisha kuwa maabara na kikafunga mlango wake, hata hivyo, jambo hilo halikutokea kamwe na hakikubadilishwa kuwa maabara.»

Wanafunzi walipouliza kama wangeweza kupewa nafasi [nyingine] kwa ajili ya kuswalia, chuo hakikujali. Wanafunzi walianza kuswali chini ya ngazi katika eneo la maegesho ya magari, lakini chuo kikasema kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa namna yoyote, mmoja wa wanafunzi alimwomba Chawki Abdullah, mkuu wa chuo, awape nafasi nyingine ya kuswalia, lakini wanafunzi waliambiwa waachane kabisa na ombi hilo.»

Takribani wanafunzi 300 hivi karibuni walitia saini kwenye waraka wa maombi, wakikitaka chuo hicho kutoa nafasi ya kuswalia kwa Waislamu, hata hivyo, Suleiman alisema kuwa wanafunzi wengi Waislamu wanaogopa kuzungumzia suala hilo kwa kuhofia kufukuzwa chuoni.

Chanzo: newarab.com

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha